Wachambuzi wa siasa za Afrika Magharibi wanasema hali hiyo inaweza kuongeza mvutano wa kisiasa nchini humo, huku mashirika ya kimataifa yakitoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa haki, huru na wa amani.

12 Oktoba 2025 - 16:55

Ivory Coast kimeumana: Wapinzani wakuu wazuiwa kugombea, Rais Ouattara atangaza kuwania muhula wa nne +Picha

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Abidjan, Ivory Coast - Joto la kisiasa nchini Ivory Coast limepanda baada ya viongozi wanne wakuu wa upinzani, akiwemo Rais wa zamani Laurent Gbagbo na Mtendaji Mkuu wa zamani wa Benki ya Credit Suisse, Tidjane Thiam, kuzuiwa kuwania katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CEI), ambayo imesema wagombea hao hawajakidhi masharti ya kisheria yanayohitajika ili kushiriki katika kinyang’anyiro hicho. Hata hivyo, wafuasi wa upinzani wamepinga hatua hiyo, wakidai kuwa ni njama ya kuwakandamiza wapinzani wa Serikali.

Wakati huo huo, Rais Alassane Ouattara, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2010, ametangaza rasmi azma yake ya kuwania muhula wa nne, licha ya kuwepo kwa utata wa kikatiba unaozunguka uamuzi huo.

Mabadiliko ya katiba ya mwaka 2016 yaliondoa ukomo wa mihula miwili ya urais, jambo ambalo limeibua mjadala mkubwa kuhusu iwapo hatua hiyo inamruhusu tena Rais Ouattara kugombea.

Ivory Coast kimeumana: Wapinzani wakuu wazuiwa kugombea, Rais Ouattara atangaza kuwania muhula wa nne +Picha

Wachambuzi wa siasa za Afrika Magharibi wanasema hali hiyo inaweza kuongeza mvutano wa kisiasa nchini humo, huku mashirika ya kimataifa yakitoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa haki, huru na wa amani.

Ivory Coast kimeumana: Wapinzani wakuu wazuiwa kugombea, Rais Ouattara atangaza kuwania muhula wa nne +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha